News

BAADA YA KUIONA MTIBWA IKIZIDI KUTITIA CHINI..MSEMAJI WAO ASHINDWA KUJIZUIA…ATAJA KINACHOWAMALIZA…

admin December 2, 2021 7:51 am


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru, anaamini kikosi chao kinapitiwa wakati wa mapito na muda si mrefu kitarejea kwenye makali yake.

Mtibwa Sugar haijapata ushindi katika michezo saba ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, huku jana Jumanne (Novemba 30) ikipoteza dhidi ya Azam FC kwa kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Kifaru amesema Uongozi wa Mtibwa Sugar kwa kushirikiana na Benchi la Ufundi unaendelea kusaka mbinu mbadala ambazo wanaamini zitawarudisha kwenye mstari wa kupata matokeo mazuri.

“Tumeanza vibaya ligi, hatujafanya vizuri kwenye mechi saba tulizocheza, Nadhani tumepitiwa na upepo mbaya tu, tunaamini tutarudi katika ubora wetu. Tunarejea katika mashamba ya miwa kujipanga zaidi.” amesema Kifaru

Kufuatia mambo kuwaendelea kombo katika michezo saba iliyopita Mtibwa Sugar inaburuza mkia wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 2.

BREAKING: CHAMA AMALIZA UTATA KUHUSU ISHU YAKE YA KURUDI TZ….AMTAJA SHOMARI KAPOMBE…. BAADA YA KUWAONA HAWAKO ‘SIRIAZI’…SAID BAHANUZI AAMUA KUWACHANA WACHEZAJI SIMBA…AMTAJA BOCCO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply