Home Simba SC HUYU HAPA ‘MIDO’ HATARI WA CONGO ANAYEZITOA UDENDA SIMBA NA YANGA…MCHAKATO UKO...

HUYU HAPA ‘MIDO’ HATARI WA CONGO ANAYEZITOA UDENDA SIMBA NA YANGA…MCHAKATO UKO HIVI…


UONGOZI wa kiungo fundi kutoka katika Klabu ya DC Motema Pembe ya nchini DR Congo, Karim Kimvuid Kiekie, umeweka wazi kuwa kwenye mazungumzo na Simba na Yanga ambazo zinahitaji huduma ya kiungo mshambuliaji huyo.

Kiekie ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 19, ni miongoni mwa wachezaji wanaotamba kwa sasa nchini DR Congo ambapo akiwa katika umri huo tayari amefanikiwa kuitumikia timu ya taifa katika michuano ya CHAN iliyofanyika mwaka jana nchini Cameroon.

Pia kiungo huyo amefanikiwa kuingia katika kikosi bora cha msimu wa Ligi Kuu ya DR Congo huku pia akishinda tuzo ya kiungo bora wa mwaka wa ligi hiyo na mchezaji bora chipukizi wa ligi hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, meneja wa mchezaji huyo, Lumingu Patrick Ntanda ambaye anamiliki kampuni ya kumiliki wachezaji ya Vestiaire 32 ambayo pia inammliki beki wa Simba, Henock Inonga Baka, ameweka wazi kuwa yupo katika mazungumzo na Simba na Yanga kuhusiana na ishu ya kuwauzia Kiekie.

“Simba na Yanga zote zinamhitaji Kiekie, nimefanya nao mazungumzo katika nyakati tofauti, Simba hii inakuwa mara ya tatu na kwa upande wa Yanga hii ni mara ya kwanza kufanya nao mazungumzo, kwa upande wa Simba mara zote tumekuwa tukishindwana katika makubaliano ya mambo ya msingi.

“Lakini safari hii Simba wameonekana kuja kivingine tofauti na mara zote, kwa upande wa Yanga kwa kuwa wao ndio mara yao ya kwanza ngoja tuone nini kitatokea lakini na wao wameonyesha nia ya kumhitaji Kiekie ambaye ukiachana na Simba na Yanga kutoka Tanzania, kuna timu nyingine ambazo zinamhitaji kutoka mataifa mengine kama Morocco na Tunisia,” alisema kiongozi huyo. 

Kwa upande wake, Kiekie akizungumzia ishu hiyo, alisema: “Nazifahamu Simba na Yanga kwa sababu kuna wachezaji wengi wa huku kwetu Congo wanacheza huko, Tanzania nimefika mara moja nikiwa na timu ya taifa, kuhusu kuhitajika huko kiongozi wangu anayenisimamia ndiye anahusika

SOMA NA HII  NABI APANIA KUITIKISA AFRIKA...ATAJA MASHINE MPYA ZA KUONGEZA NGUVU YANGA...