News

SAA CHACHE KABLA KUCHEZA NA WAZAMBIA WENZAKE…BWALYA AFANYA MAAMUZI MAGUMU KISA SIMBA…

admin December 5, 2021 11:32 am

 


Kiungo mshambuliaji Rally Bwalya, amesema atajitoa kuhakikisha anaisaidia Simba SC kufanya vizuri dhidi ya Red Arrows kesho ili kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kucheza kwenye ardhi ya nyumbani kwao Zambia.

Bwalya amesema Simba ni waajiri wake na siku zote ataipa nafasi ya kwanza katika kila kitu kama mkataba wake unavyoeleza.

“Ninasikia furaha kucheza katika ardhi ya nyumbani, naipenda nchi yangu lakini nimekuja kikazi nitahakikisha naisaidia Simba kupata ushindi ili tuingie hatua ya makundi,” amesema Bwalya.

Akizungumzia mchezo wa leo Bwalya amesema itakuwa mgumu lakini tupo tayari kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

“Kama alivyosema kocha, mechi itakuwa ngumu, tunajua Red Arrows wataingia kwa nguvu kutafuta mabao lakini sisi ni Simba tutakuwa tayari kuwakabili,” amesema Bwalya.

MASHABIKI FENERBAHCE WATAKA ALIYERUHUSU SAMATTA  AUZWE AFUKUZWE HARAKA….OZIL ATAJWA.. KAGERE, MORRISON KUIONGOZA SIMBA DHIDI YA RED ARROWS..INONGA KAMA KAWA, KAPOMBE BENCHI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply