News

BAADA YA KUIONA SIMBA ILIVYOCHEZA JANA…’TRY AGAIN’ AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA…AITAJA YANGA..

admin December 6, 2021 1:00 pm

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema kikosi chao kipo tayari kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans utakaopigwa Jumamosi (Desemba 11) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

‘Try Again’ ametoa kauli hiyo akiwa mjini Lusaka, Zambia ambako kikosi cha Simba SC jana Jumapili (Desemba 05) kilikabiliwa na mchezo wa Mkondo wa Pili wa Kombe la Shiriksiho Afrika dhidi ya Red Arrows.

Kiongozi huyo amesema kikosi chao msimu huu kipo tayari kwa mchezo wowote, huku akiwatoa hofu Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuelekea Jumamosi (Desemba 11).

“Niwatoe wasiwasi Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, timu yao ni nzuri, inaweza kukabiliana na yoyote msimu huu, tunakwenda kucheza na timu ya kawaida ambayo ipo kwenye Ligi kama ilivyo kwa timu nyingine,”

“Sioni shaka, Sioni wasiwasi kwa nini tunazungumzia mchezo unaofuata, huo ni mchezo kama mchezo mwingine wowote wa Ligi tuliowahi kucheza ama tutakaocheza msimu huu.”

Hakuna sababu ya kuhofia, sisi Simba SC sio watu wa tambo wala Sio watu wa kujivuna, lakini tunachosema ni kwamba tunakwenda kushinda mchezo huo. Sisi kila mchezo ambao tunakutana na mpinzani yoyote tunahakikisha kwamba tunashinda.” amesema Try Again.

Simba SC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 17, ikitanguliwa na Young Africans yenye alama 19, huku kila timu ikicheza michezo saba hadi sasa.

YANGA IKIJINDAA DHIDI YA SIMBA…MWAKALEBELA AFICHUA SIRI JINSI WATAKAVYOSHINDA NNJE YA UWANJA.. KUELEKEA KARIAKOO DABI…SIMBA KUWACHAJI MASHABIKI WA YANGA TSH 30,000..ISHU NZIMA IKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply