News

KUELEKEA SIMBA vs YANGA…POLISI YATOA TAMKO..WANAONG’OA VITI NA KUINGIA NA VISU KUKIONA..

admin December 10, 2021 8:53 am


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limejipanga kikamilifu kuhakikisha ulinzi unaimarishwa kwa kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga siku ya tarehe 11/12/2021 majira ya saa kumi na moja jioni katika Uwanja wa Benjamini Mkapa lengo ni kuwafanya mashabiki wa mpira wa miguu watakaoshuhudia mchezo huo wawe kwenye mazingira ya Amani na Utulivu.

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam halitatoa fursa kwa mtu/watu wenye lengo la kufanya vurugu katika mchezo huo na kuharibu miundo mbinu ya uwanja kwa sababu yeyote ile.

 Pia Jeshi linapiga marufuku kwa mtu yeyote yule asiyehusika na mambo ya kiusalama kuingia uwanjai na silaha yoyote ikiwa ni pamoja na silaha za moto, visu, Panga au mawe kwa kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa.

Simba na Yanga zitakutana kesho kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam na mshindi wa mechi hiyo ndiye ataongoza kwenye msimamo ambao sasa Yanga ndio kinara ikiwa na pointi 19 na Simba ni ya pili na pointi 17.

MWAKA TUNAUFUNGA HIVI NA SIMU INAYOKAA NA CHAJI KWA ZAIDI YA  MASAA 72. KUELEKEA KARIAKOO DABI…PABLO BAADA YA KUITAZAMA SIMBA YAKE..AGUNA KISHA ATOA KISINGIZIO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply