Azam FC

WAKATI PRINCE DUBE AKIRUDI ….NADO NNJE MIEZI TISA

admin December 15, 2021 4:00 pm


WINGA machachari wa Azam Fc, Idd Seleman ‘Nado’ atakuwa nje ya uwanja kwa miezi tisa baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini katika hospitali ya Vicent Pallot.

Nado aliondoka nchini jana (Jumanne) alfajiri na kwenda Afrika Kusini kwenda kufanyiwa vipimo kwa mara ya pili kisha alifanyiwa upasuaji.

Kupitia taarifa iliyotolewa na ukurasa wa rasmi wa Instagram  imeeleza ;”Daktari wetu Mwanandi Mwankemwa amethibitisha mshambuliaji wetu Idd Seleman ‘Nado’ atakuwa nje dimba kwa miezi tisa akiuguza majeraha yake ya kukatika mtulinga wa kati wa mguu wake wa kulia.”

Licha ya mchezaji huyo kukosekana katika timu hiyo, mshambuliaji wao mwingine Prince Dube alirejea  uwanjani kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.

Nado aliumia katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao walishinda 1-0 uliochezwa Novemba 30 katika uwanja wa Azam Complex.

ISHU YA UWANJA MPYA SIMBA  NA AHADI YA MO YACHUKUA SURA MPYA…’KIGOGO’ AFUNGUKA YA NDANI…. BAADA YA KUONA KINA KAGERE ‘WAKIRUKA RUKA’ BILA KUFUNGA..PABLO AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply