News

WAKATI MAKAMBO AKIANZA KUTUPIA YANGA…MAYELE APATA ‘PANCHA’..AINGIA UWANJANI AKICHECHEMEA…

admin December 16, 2021 4:00 am


Staa wa Yanga Fiston Mayele ni miongoni mwa watazamaji waliofika  jana Uwanja wa Benjamini Mkapa kushuhudia mchezo wa FA kati ya Yanga na Ihefu.

Mayele aliingia jukwaa kuu wakati mpira ni mapumziko na baada ya kuingia alisogea kusalimiana na baadhi ya viongozi wa Yanga.

Lakini wakati anatembea kuwasogelea viongozi hao alikuwa akichechemea kuashiria kwamba ana maumivu kwenye mguu wake.

Hali hiyo alionekana nayo pia wakati anaotembea kwenda kuketi kwenye kiti chake kwa ajili ya kutazama mechi.

Katika mchezo huo, Yanga waliweza kupata ushindi mnono wa magoli manne kwa bila, huku mshindani wa  Mayele kwenye kikosi cha Nabi, Herieth Makambo akifunga magoli matatu.

WAKATI CHAMA AKIWA HURU SASA…YANGA WAANZA KUPIGA DANADANA KUHUSU KUMSAJILI…NABI ATAJWA…. PAMOJA NA KUFUNGWA NA SIMBA..KOCHA WA JKT TANZANIA ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA HAYA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply