News

KISA MECHI YA KAGERA vs SIMBA KUGHAIRISHWA…MANARA ATUPA DONGO ZITO MSIMBAZI…

admin December 19, 2021 4:54 am


Baada ya kutoka kwa taarifa ya mechi ya Kagera na Simba kuahirishwa kwa sababu ya wachezaji wa Simba kuumwa mafua na kifua, Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amewaombea wachezaji wa klabu hiyo ili kuendelea na majukumu yao.

Kupitia Instagram yake Haji Manara ameandika kuwa; “Maradhi yanapowatokea wenzenu hata kama mna upinzani gani lazima uwaombee dua wapone haraka,ili waweze kurudi kucheza tena. 

“Nimeyanukuu maneno ya King Pele alipowaombea wachezaji nyota wa Sweden walioumwa mafua,kabla ya mechi ya fainali ya kombe la dunia baina ya Waswidish na Wabrazil World Cup ya 1958 kule Stockholm.

“Na sisi wadau wa soka tunawaombea wachezaji wa Simba wapone haraka ili warejee uwanjani tena. Mimi siamini zile za ndani eti sijui mishahara sijui bonus ya kutoka sare na Yanga, naamini wenzetu wamepata maradhi na Insha’Allah watapona,” ameandika Manara.

SIMBA CHINI YA ULINZI MKALI…MABOSI WAIGOMEA GSM..KIUNGO SIMBA ATUA AZAM… PAMOJA NA KUANZA VYEMA SIMBA…PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA MSIMAMO WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply