Azam FC

BAADA YA KUTOKA SARE NA MBEYA CITY…MAKOCHA WAPYA AZAM WAVUNJA UKIMYA…WATAJA MABADILIKO…

admin December 22, 2021 7:00 am


KAIMU kocha msaidizi mpya wa Azam, Mohamed Badru ameweka wazi kuwa benchi lao la ufundi linahitaji muda zaidi ili kusuka kikosi kitakachokuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri ya ushindi.

Azam Jumatatu iliyopita walitangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha wao Mzambia, George Lwandamina ambaye aliuandikia barua Uongozi wa klabu hiyo akiomba kujiuzulu na nafasi hiyo kuchukuliwa na mkurugenzi wa ufundi, Abdihamid Moalin huku Mohamed Badru akikaimu nafasi ya kocha msaidizi.

Badru juzi Jumamosi alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Azam lililoiongoza klabu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ulioisha kwa sare ya mabao 2-2.

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha msaidizi wa Azam, Mohammed Badru alisema: β€œTunashukuru kwa matokeo ya sare ambayo tuliyapata kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya Mbeya City licha ya kwamba haukuwa mpango wetu.

β€œLicha ya kwamba hatukupata ushindi, lakini tunajivunia mabadiliko makubwa ambayo kikosi kimeyaonyesha mpaka sasa, tunaamini tukipata muda zaidi wa kuwa pamoja basi tutarejesha ari yetu ya ushindi.”

RASMI…’SURE BOY’ ABANDIKWA MIAKA MIWILI YANGA..AZAM WASALIMU AMRI…MWAKALEBELA AMTAJA NABI… HUYU HAPA KIUNGO MCONGO ‘MKATA UMEME’ ANAYEZIGOMBANISHA SIMBA NA YANGA..ISHU NZIMA IKO HIVI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply