Home BIashara United KWA HILI TU…NABI HATANII…HADI HUYU..? …RIPOTI YAKE NZITO YAANIKA KILA KITU…

KWA HILI TU…NABI HATANII…HADI HUYU..? …RIPOTI YAKE NZITO YAANIKA KILA KITU…


MABOSI wa Yanga wako katika vikao vya siri wakipiga hesabu za usajili kupitia dirisha dogo lililofungwa Desemba 16, lakini ripoti ya kocha wao Nesreddine Nabi imewekwa bayana ikitaka mashine mpya nne za haraka na tayari uhakika kuna mastaa wawili wameshaanguka sahihi zao.

Pamoja na kuwa na uhakika wa Salum Abubakar na Denis Nkane, Nabi ametaka pia beki mmoja wa kati atakayewapa presha nahodha Bakar Mwamnyeto na Dickson Job wanaocheza kwa sasa wakipigwa tafu wakati mwingine na Yannick Bangala anayemudu pia kucheza kama kiungo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, inayosimamia pia usajili, Dominic Albinius alisema kuwa, wamepokea ripoti ya Nabi na tayari imeshaanza kufanyiwa kazi kwa utulivu mkubwa kwenye dirisha dogo la usajili litakalofungwa Januari 15.

Albinius, ambaye kitaaluma ni kocha wa soka alisema katika kutengeneza safu bora ya ulinzi kocha wao, bado anataka aletewe beki wa kati atakayekuja kushindana na nahodha Bakari Mwamnyeto na Dickson Job. Mbali na Job na Mwamnyeto eneo hilo pia lina Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Bangala anayemudu kucheza pia eneo la kiungo mkabaji.

Aidha katika eneo hilo kuna uwezekano baadhi ya mabeki kutolewa kwa mikopo na kuachwa kulingana na mikataba yao.

Albinius alisema pia ripoti hiyo inataka viungo wawili tofauti mmoja wa pembeni anayeziba pengo la Yacouba Songne aliyefanyiwa upasuaji na atakosa msimu mzima, pia akitakiwa kiungo mshambuliaji wa kati .

“Tunamtafutia pia kiungo mshambuliaji wa kati atakayekuwa mbunifu zaidi unajua mpaka sasa eneo hilo kuna Feisal Salum pekee wakati huu Mapinduzi Balama akiendelea kutafuta ubora wake akitokea majeruhi,” alisema Albinius.

Mmoja ya mabeki wanaotajwa kuingia kwenye rada za Yanga ni Abdulmajid Mangalo aliyepo Biashara United, pia jina la Kulwa Idd Mobby, aliyepo Geita Gold likitajwa.

Albinius, aliongeza Nabi amehitaji mshambuliaji mwingine mwenye kasi ya kufunga zaidi atakayekuja kushindana na Fiston Mayele na Heritier Makambo.

“Nabi anahitaji mtu wa namna hiyo atakayekuja kushirikiana na Mayele na Makambo, si mnajua Yusuf (Athuman) ameumia tunapambana kumtibu, lakini wakati huu ni vyema tukapata mtu bora.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUTUA CHATO...KMC WATEMBELEA KABURI LA MAGUFULI...WAWEKA HISTORIA YA MAPOKEZI...

Albinius alisema kazi ya kutafuta wachezaji hao inafanywa kwa umakini mkubwa na kila mchezaji wanayemtaka hujadiliwa na kamati yao, kisha kocha kushirikishwa kuangalia ubora wake wa huko anakotoka na kipi kitasaidia timu yao.

“Hapa Yanga usajili haufanywi na mtu mmoja, tupo kama kamati ya ufundi yenye watu bora, pia kocha wetu (Nabi) anahusika kuangalia ubora, ilio kupata wa kuisaidia timu. Tukimaliza kazi mtatangaziwa,” alisema.