News

WAWA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AANIKA WAZI MAHUSIANO YAKE NA PABLO..ATAJA TOFAUTI ZAO..

admin December 29, 2021 12:00 pm


Sergio Wawa, beki wa kati wa Simba, ameweka wazi kuwa hakuna tofauti kati yake na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco.

Ijumaa iliyopita katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora ilitokea hali ya kutoelewana katika suala la kufanya mabadiliko ambapo Wawa alikuwa anajiandaa kuingia uwanjani akitokea benchi ghafla, Pablo alimvuta kwa nguvu kubwa na kuonekana akilalamika.

Pia Pablo alionekana mwenye hasira ambapo alionekana akipiga kiti na chupa ya maji jambo ambalo liliweza kuonesha kwamba alikuwa amekasirika kwelikweli.

Kutokana na kitendo hicho ilibidi Wawa arudi benchi na kumaliza dakika 90 akishuhudia mchezo huo ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma KMC 1-4 Simba.

Wawa amesema kuwa hakuna tofauti kati yake na kocha wa timu hiyo. β€œHakuna tofauti kati yetu na kocha kila kitu kinakwenda vizuri na tunashukuru kwa kuwa tumeshinda,” alisema Wawa.

KWA TAARIFA YAKO..ILE ISHU YA CHAMA KURUDI TZ…IKO SAWA SAWIA NA ISHU ZA OKWI KURUDI SIMBA… BAADA YA KUSAINI  TU …’SURE BOY’ APEWA JEZI YENYE GUNDU ..KILA ALIYEIVAA HAKUDUMU NA YANGA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply