Burudani

KISUBI AVUNJA UKIMYA SIMBA…ATOA KAULI NZITO AKISEPA KUJIUNGA NA MTIBWA…ADAI UTU WAKE….

admin December 31, 2021 5:00 pm


ALIYEKUWA kipa wa Simba SC, Jeremiah Kisubi amewashukuru uongozi na mashabiki wa klabu hiyo kwa kipindi alichohudumu huku akisema kuwa, ameamua kufanya maamuzi ya kuondoka msimbazi ili kulinda utu wake.

Kisubi ambaye ametimkia Mtibwa Sugar kwa mkopo amesema; “Sijazoea kuishi chini ya kivuli mara zote naamini ninachokifanya. Na Mungu atailinda heshima yangu iliyoshushwa kilazima.

“Nawapenda napenda kila kitu kutoka kwenu naheshimu ukubwa wa klabu nawatakia kila kilicho chema tutaishi milele kwa kuwa mimi bado ni sehemu yenu. Ila utu wangu ni bora kuliko kitu,” amesema Kisubi.

Kisubi ambaye alijiunga na Simba katika dirisha kubwa la usajili wa msimu huu mnamo Agosti 18, mwaka huu akitokea Tanzania Prisons ya Mbeya amekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba jambo ambalo limepelekea kuandika barua kwa uongozi wa timu hiyo kuomba kutolewa kwa mkopo kwenda Mtibwa

BAADA YA KUONA ‘MAVITU’ YA SURE BOY MAZOEZINI…NABI ATIKISA KICHWA..KISHA AKASEMA HAYA … FT: YANGA 4-0 DODOMA JIJI….MAYELE KAMA KAWA…’FEI TOTO’ AACHA MSALA DODOMA JIJI …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply