Home news ALIYETUPIA ‘HAT TRICK’ ATUMA SALAMU YANGA…ATOA ONYO KUHUSU MTEREMKO….

ALIYETUPIA ‘HAT TRICK’ ATUMA SALAMU YANGA…ATOA ONYO KUHUSU MTEREMKO….


Mshambuliaji wa Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ Jeremiah Juma ameitumia salamu Young Africans, ambayo kwa sasa ipo safari kuelekea mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Young Africans itakua mgeni wa Maafande hao keshokutwa Jumapili (Desemba 19) katika Uwanja wa Nelson Mandela.

Jeremiah ambaye mpaka sasa ndiye mchezaji pekee aliyefunga Hat Trick kwenye Mshime Mshike wa Ligi kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22 amesema: “Yanga wasitarajie mteremko, tunawasubiri kwa hamu tuliwaona kwenye mechi zao, lakini niwaombe mashabiki waje kwa wingi waone pira gwaride, tutakomaa na kuweka rekodi Jumapili.”

Tanzania Prisons itakwenda kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Young Africans, ikiwa nafasi ya 13 katika Msimamo wa Ligi hiyo kwa kufikisha alama 8, huku wageni wao wakiwa kileleni kwa kumiliki alama 20.

SOMA NA HII  TSHABALALA, KAPOMBE WAMKOSHA GOMES...ATOA AHADI KUBWA ...