Home news BAADA YA KUZIDI ‘KUKICHAFUA’ NA AL AHALY…MIQUISSONE AINGIA ANGA ZA SAMATTA..

BAADA YA KUZIDI ‘KUKICHAFUA’ NA AL AHALY…MIQUISSONE AINGIA ANGA ZA SAMATTA..


Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Jose Luis Miquissone ameweka Rekodi ya kuwa sehemu ya wachezaji waliotwaa ubingwa wa CAF Super Cup akiwa na mabingwa wa Afrika Al Ahly.

Miquissone ambaye aliitumikia Simba SC kabla ya kuondoka mwanzoni mwa msimu huu, ameweka Rekodi hiyo usiku wa kuamkia leo, baada ya Al Ahly kuichapa Raja Casablanca kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.

Mchezo uliochezwa Uwanja wa Al Rayyan nchini Qatar, ulishuhudia miamba Al Ahly na Raja Casablanca walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, ambapo kwa Al Ahly Taher Mohamed alisawazisha bao dakika ya 90 ambalo Yasser Ibrahim alijifunga dakika ya 13.

Kwa upande wa mikwaju ya Penati ambayo iliamua mshindi Al Ahly katika fainali walipachika mikwaju 6 huku Raja Casablanca wakiwa wametupia mikwaju 5.

Kwa mafanikio hayo Luis Miquissone anakuwa miongoni mwa wachezaji waliowahi kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara na kubeba taji la Afrika ngazi ya klabu.

Wengine ambao wamewahi kufanya hivyo ni pamoja na Mbwana Samatta ambaye alikuwa anakipiga Simba SC kisha akaibukia TP Mazembe.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU