Home news SIMBA YAACHA WACHEZAJI TISA….BOCCO, NYONI, WAWA NA KISUBI WATAJWA…

SIMBA YAACHA WACHEZAJI TISA….BOCCO, NYONI, WAWA NA KISUBI WATAJWA…


Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC itakosa huduma ya wachezaji Tisa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar, utakaopigwa kesho Jumamosi (Desemba 18).

Simba SC wamesafiri kulekea mjini Bukoba mkoani Kagera kusaka alama tatu za mpambano huo, ambao utaunguruma kuanzia saa 10:00 jioni, Uwanja wa Kaitaba.

Meneja wa Simba SC, Patrcik Rweyemamu amesema wachezaji tisa wameachwa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kuwa majeruhi, kuugua na matatizo ya kifamilia, lakini kikosi kilichotua jana Alhamis (Desemba 16) Jioni mjini Bukoba kipo tayari kupeleka moto kwa Kagera Sugar na kuendeleza wimbi lao la ushindi.

Wachezaji walioachwa jijini Dar es salaam ni Bernard Morrison, Rally Bwalya, John Bocco, Chris Mugalu, Taddeo Lwanga, Erasto Nyoni, Jeremiah Kisubi, Israel Mwenda na Pascal Wawa.

SOMA NA HII  HAZIRA ZA SOPU ZAHAMIA KWA MANULA WA SIMBA...DENI LAKE LAZIDI KUKUA KILA SIKU....