Home news WAKATI AKISEMWA KUWA NA KIWANGO KIBOVU…WAWA AVUNJA UKIMYA SIMBA…ADAI ATAONDOKA…

WAKATI AKISEMWA KUWA NA KIWANGO KIBOVU…WAWA AVUNJA UKIMYA SIMBA…ADAI ATAONDOKA…


BEKI mkongwe wa Simba, Pascal Wawa amesema siri kubwa ya yeye kurejea kikosi cha kwanza imetokana na kujitambua katika kupigania kiwango chake muda wote ili kuweza kucheza timu hiyo.

Wawa aliondolewa kikosi cha kwanza baada ya Simba kufungwa bao 3-1 na Jwaneng Galaxy huku akionekana kuonyesha kiwango cha kawaida hali iliyowafanya baadhi ya viongozi kuchukizwa na matokeo hayo na kuchukua uamuzi wa kufumua Benchi la Ufundi chini ya kocha mkuu Didier Gomes aliyetimuliwa.

Baada ya mabadiliko hayo, uongozi wa Simba ulimteua Kocha Thiery Hitimana kukaimu nafasi hiyo ambaye alimtoa kikosini mkongwe huyo mechi tatu mfululizo dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, Namungo lakini ujio wa kocha mpya Pablo Franco umemrejesha kikosi cha kwanza.

Akizungumza hivi karibuni, Wawa alisema “Kwangu ninachokifanya ni kujitolea kwa ajili ya timu hadi pale muda wangu wa kuondoka ukifika, ninajivunia kuwa hapa kufanya kile ambacho Mungu amenibariki ili nikifanye.”

Alisema anatambua wapo watu wanaomsema vibaya lakini haimpi shida wala kumkatisha tamaa badala yake anaendelea kuifanya kazi yake kwa nguvu nyingi.

Wawa ambaye anaonekana kama umri wake umeenda amekuwa na kawaida ya kuaminiwa na makocha mbalimbali ndani ya Simba kuanzia Patrick Aussems hadi sasa Pablo Franco.

SOMA NA HII  GAMONDI KUWABADILISHAI 'GIA ANGANI' AL AHLY.....MPANGO MPYA WASUKWA KIMYA KIMYA...