news

HAO YANGA WASIKIENI TU HIVYO HIVYO…KAZE AANIKA BALAH JIPYA…WAITAJA SIMBA…

admin January 1, 2022 12:00 pm


VINARA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga, wametamba wako imara na kamili kuendelea kutoa ‘dozi’ kwa kila timu watakayokutana nayo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, amesema kuwa wanakwenda Zanzibar na wachezaji wao wote isipokuwa ambao ni majeruhi kwa sababu wanataka kurejea na ubingwa wa michuano hiyo.

Kaze alisema kila mchezaji wa Yanga anafahamu malengo waliyokuwa nayo msimu huu, hivyo wameahidi kuhamishia ‘makali’ yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye mashindano hayo.

“Tunataka kuendelea kufanya vizuri katika kila mashindano tunayoshiriki, kikosi chetu kimeimarika na kiko tayari kwa ajili ya kupata ushindi,” alisema Kaze.

Aliongeza kila mechi kwao sasa ni sawa na fainali kwa sababu wanataka kukaa kileleni na si kwenye nafasi za chini.

“Tumejiandaa kukutana na ushindani, tunajua tutakutana na timu zilizojipanga pia, mechi zetu zote ni sawa na fainali, tunaingia kwa ajili ya kusaka ushindi tu,” alisema Kaze.

Katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Yanga imepangwa Kundi B ikiwa pamoja na Taifa Jang’ombe na KMKM wakati Simba iko Kundi C na Selem View na Mlandege wakati Kundi A linaundwa na Azam FC, Namungo, Yosso Boys na Meli 4 City.

Yanga ambayo ilitolewa mapema katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, pia inashiriki michuano ya Kombe la FA.

BAADA YA KUTEMANA NA SIMBA…HITIMANA AANIKA SIRI ZA MKUDE..AFICHUA ALIVYOMFUNDA… KUELEKEA MICHUANO YA CAF…KIGOGO SIMBA AFICHUA MIPANGO YA KIMAFYA..WAZITAKA MECHI MBILI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply