UKISEMA wa nini wenzako wanajiuliza watampata lini. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mbeya City ambapo inaelezwa kuwa imeonyesha nia ya kumsajili aliyekuwa kipa namba tatu wa Yanga, Ramadhan Kabwili.
Chanzo kutoka Yanga, kimesema kuwa: “Wakati viongozi walipokuwa katika mchakato wa kumuondoa Ramadhan Kabwili kikosini, kuna klabu ya ligi kuu ilikuwa imetuma barua ya kuhitaji huduma yake.
“Barua ililetwa Jangwani kutoka Klabu ya Mbeya City ambayo imeonesha nia ya dhati kabisa ya kuhitaji huduma ya Kabwili.
Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kuzungumzia hilo, alisema: “Masuala ya usajili yatakapokamilika yatawekwa wazi na klabu, lakini mpaka sasa tumeshamtangaza wachezaji tuliosajili na kuwaacha”.