news

USAJILI WA NKANE YANGA WAZUA JAMBO…UONGOZI WAGUSIA KUTEMA MCHEZAJI…

admin January 3, 2022 1:00 pm


Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema hana budi kumtoa kwa mkopo kiungo mmoja katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.

Nabi ameweka wazi mpango huo kabla ya kuondoka nchini kuelekea Ubelgiji kujiunga na familia yake kwa mapumziko katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu imesimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Kocha huyo kutoka Tunisia amesema usajili wa kiungo Dennis Nkane aliyetokea Biashara United Mara unamsukuma kufanya maamuzi hayo ya kumpunguza mchezaji mmoja.

“Kwa sasa tutakuwa na jumla ya mawinga watano, naangalia uwezekano wa kumtoa mmoja ili timu iwe na uwiano mzuri tubaki na wanne.”

Mbali na Nkane, mawinga wengine ni Farid Mussa, Dickson Ambundo, Jesus Moloko na Deus Kaseke

MORRISON, MANULA NA ONYANGO OUT SIMBA….LWANGA NDANI SAFARI YA SIMBA ZANZIBAR… NABI AAMUA KUSEPA YANGA…CHANZO HIKI HAPA…KAZE ATAJWA…UONGOZI WABARIKI…..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply