Winga kinda Denis Nkane ameanza vizuri maisha yake ndani ya kikosi cha timu ya Wananchi Yanga SC baada ya hapo jana kufungwa bao 1 kwenye mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na kikosi hicho, kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi ambao Yanga iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Taifa Jan’gombe
Nkane alifunga bao la pili kwenye ushindi huo wa mabao 2-0 ambapo bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Haritier Makambo, Yanga wakianza safari ya kutetea ubingwa wa michuano hiyo kwenye mchezo huo wa kundi B.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 18 pia amekabidhiwa jezi namaba 16 ambayo iliwahi kuvaliwa na Mrisho Khalfani Juma Ngasa moja kati ya mawinga hatari waliowahi kukitumikia kikosi hicho na Nkane binafsi aliwahi kunukuliwa akisema katika ukuaji wake kwenye mchezo wa Soka Mrisho Ngasa ni moja kati ya wachezaji ambao alikuwa akiwaangalia sanaa na kujifunza baadhi ya vitu kutoka mchezaji huyo.
Denis Nkane amejiunga na Yanga akitokea katika klabu ya Biashara Mara United kwa mkataba ambao haukuwekwa wazi ni wa muda gani na alikuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa katika dirisha dogo la usajili baada ya mlinda mlango kutokea Mtibwa Sugar Abdultwalib Mshery na kiungo Salum Abubakari ‘Sure Boy’ kutoka Azam Fc kabla ya usajili wa mshambuliaji Crispin Ngushi kutoka Mbeya Kwanza.