News

HUKU USAJILI WAKE UKINGOJEWA KWA HAMU…CHAMA AIBUKA NA KUTOA KAULI TATA…

admin January 12, 2022 9:00 am


Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chama ‘Triple C’ ameendelea kuwaweka njia panda wadau wa soka nchini kufuatia tetesi zinazoendelea kuwa, huenda akarejea kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Chama ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa nchini kwao Zambia kwa mapunziko, amekua anahusishwa na mpango wa kusajiliwa Simba SC katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, ambacho kitafikia kikomo Januari 15.

Kiungo huyo amesema: “Kama ambavyo Simba walikubaliana na RS Berkane nikaondoka kwao, nadhani unahitajika muda mwingine wa kufanya uamuzi kama huo kutambua kama nitakuja Tanzania au kubaki kule Morocco.”

Chama aliuzwa RS Berkane mwishoni mwa msimu uliopita akitokea Simba SC, lakini taarifa zinaeleza kuwa mazingira ya Morocco yamekua magumu kwake, hivyo amelazimika kuvunja mkataba wake na wakati wowote atarejea Msimbazi.

WAKATI YANGA WAKIMTUPIA NDOANO YA USAJILI…PABLO ASHTUKA JAMBO..AAGIZA MNIGEIA ASAJILIWE CHAP… SIMBA KWELI NI BABA LAO…BODI YA LIGI YABADILI RATIBA KISA CAF…YANGA KAMA KAWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply