Home news KISA YANAYOENDELEA …NABI ARUDI BONGO CHAP..ATOA KAULI NZITO YANGA…

KISA YANAYOENDELEA …NABI ARUDI BONGO CHAP..ATOA KAULI NZITO YANGA…


Kocha wa Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi ametua jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo Alhamis (Januari 13), akitokea Ubelgiji alipoa amekwenda kwa mapumziko.

Kocha huyo kutoka nchini Tunisia aliondoka nchini mwanzoni mwa mwezi huu, huku akikabidhi kikosi cha Young Africans kwa msaidizi wake Cedric Kaze, ambaye alikiongoza kwenye michuano ya Mapinduzi 2022.

Baada ya kutia nchini Kocha huyo ataanza kazi ya kukinoa kikosi chake, kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo kitacheza ugenini dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania.

Tayari kocha huyo amewaasa viongozi wa klabu hiyo kuwaamuru wachezaji warudi kambini haraka kwa baadhi ya wachezaji waliopo mapumzikoni, kwani kilichotokea kwenye michuano ya Mapinduzi hakikumfurahisha na hakitoi nafasi ya kupumzika.

Nabi amewaambia Mabosi wa Young Africans kutokana na anguko la kikosi chake kwenye Kombe la Mapinduzi hakuna haja ya mapumziko marefu, kwani kuna michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania, ambayo ameitabiria kuwa na upinzani mkubwa.

Young Africans itaanzia Jijini Tanga Januari 16 kucheza dhidi ya Coastal Union, kisha itaelekea mkoani Kilimanjaro kupepetana na Polisi Tanzania.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 29, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 24 huku Polisi Tanzania ikiwa nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 17.

SOMA NA HII  BAADA YA KUISASAMBUA IHEFU JANA...MBRAZILI SIMBA ATAJA MKAKATI WA KUMALIZANA NA YANGA...