News

BAADA YA KUUONA MZIKI WA SIMBA UKITUA JANA MBEYA UKIWA NA CHAMA NDANI..MBEYA CITY WAOMBA SARE TU…

admin January 16, 2022 9:13 am


KUELEKEA mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba, benchi la ufundi la Mbeya City limetamba kuwa licha ya ubora walionao wapinzani wao lakini watahakikisha wanapata ushindi.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa Januari 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Akizungumza hivi karibuni, Meneja wa Mbeya City, Mwegane Yeya, alisema: “Tunaendelea na maandalizi kuelekea kwenye mchezo wetu wa ligi dhidi ya Simba.

“Tunajua Simba wana timu nzuri, wachezaji wazuri kutokana na ubora waliouonyesha kwenye michuano ya Mapinduzi lakini hata sisi pia tuna kikosi bora, hivyo tutahakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huo.

“Utakuwa mchezo mgumu lakini sisi haitutishi, tutahakikisha tunautumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani kwa kupata pointi tatu kama ikishindikana basi tupate pointi moja kuliko kupoteza.”

SHIBOUB NDIYO BASI TENA MSIMBAZI…PABLO AKUNJA SHINGO…AHMED ALLY ATOA MSIMAMO WA KLABU… KIUNGO YANGA ASHINDWA KUJIZUIA KWA MAVITU YA SAKHO…AMATABIRIA MAKUBWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply