Home news KISA KICHAPO TOKA YANGA…COASTA UNION WAKOSA MAMILIONI YA TSH…MKUU WA MKOA ATAJWA…

KISA KICHAPO TOKA YANGA…COASTA UNION WAKOSA MAMILIONI YA TSH…MKUU WA MKOA ATAJWA…


WACHEZAJI wa Coastal Union, waliahidiwa kuondoka na kiasi cha shilingi milioni 50 kama wangeendeleza ubabe kwenye uwanja wa Mkwakwani kwa kuifunga Yanga, lakini imeshindikana baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ulichezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa.

Ahadi hiyo waliyopewa wachezaji wa Coastal Union ilitoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima ambaye aliahidi shilingi milioni 20, Mbunge wa Jimbo hilo, Ummy Mwalimu naye akiahidi milioni 10, huku milioni 20 zingine zikitoka kwa mdau mmoja wa soka ambaye hakupenda kutajwa jina lake.

 Nahodha wa Coastal Union, Mtenje Albano, alisema wanajua wamewakwaza mashabiki wao kutokana na kutowapa raha ya ushindi, lakini hakusita kuwapa matumaini akisema bado wako imara akiwaahidi kuwatuliza na kuwarudishia furaha watakapokutana na Namungo katika mchezo unaofuata utakaochezwa uwanjani hapo.

“Tulijiandaa vizuri tukiamini tutachukua pointi tatu, lakini tulishindwa kutumia nafasi tulizozipata, niwatake tu mashabiki wasikate tamaa, waendelee kutuamini, tunawaahidi kufanya vizuri zaidi,” alisema nahodha huyo.

Kwa upande wa Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, alisema mwendo wao wa kushinda michezo yote msimu huu katika ligi kuu bado uko na makali yaleyale, huku wakizidi kuimarika kila siku.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIJITAFUTA...SIMBA WAZIDI KUTOBOA KIMATAIFA...WAINGIA KWENYE ANGA LA TIMU KUBWA DUNIANI...