News

WAKATI JAHAZI LA SIMBA LIKIPATWA NA DHORUBA..PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..ALIA NA RATIBA..

admin January 24, 2022 2:30 pm


PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba, amesema wana ratiba ngumu jambo linalowafanya kutumia nguvu kubwa kusaka ushindi.

Juzi Jumamosi, Simba ilicheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na mcheo kuisha kwa timu zote kugawana alama moja.

Kabla ya mchezo huo, Simba ilitoka kupoteza mbele ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0.

Jumatano ijayo watakuwa mkoani Kagera kupambana na Kagera Sugar. Hizi ni mechi za ligi kuu. Kisha Januari 30, watawakaribisha Dar City kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya 32 bora.

Pablo amesema: “Tumetoka Mbeya kucheza, kisha Mtibwa Sugar, baada ya hapo bado tuna kazi nyingine, ratiba bado inaonesha kwamba wachezaji wanapaswa kucheza muda wote.

“Katika hilo wapo wachezaji ambao ilinipasa kuwapumzisha ikiwa ni pamoja na Rally Bwalya ambaye alikuwa amechoka, hivyo tuna kazi kubwa yakufanya katika mechi zetu zijazo.”

KURUDI KWA CHAMA….HAYA HAPA MAMBO MATANO MAKUBWA ALIYORUDI NAYO BONGO… BAADA YA KUUONA UCHEZAJI WA USHINDI…NABI AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA…ATAJA PRESHA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply