News

PAMOJA NA KUSOTA BENCHI …MAKAMBO AVUNJA UKIMYA YANGA…AFUNGUKA KUHUSU YANAYOMKUMBA…

admin January 25, 2022 9:34 am


HERITIER Makambo, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ipo siku atafunga kwenye ligi kwa kuwa ni suala la muda hana mashaka nalo.

Kwenye ligi Yanga ikiwa imefunga mabao 22 katika mechi 12 ambazo imecheza, nyota huyo raia wa DR Congo hajafanikiwa kufunga wala kutoa pasi ya bao.

Akizungumza na gazeti la  Championi  Makambo alisema kuwa anatambua kwamba mashabiki wanapenda kuona akifunga ila muda bado haujafika.

“Mashabiki wanapenda kuona nafunga hata mimi pia ninapenda kufanya hivyo lakini ni suala la kusubiri kwani bado kuna mechi za kucheza na mechi zipo nyingi hivyo ipo siku nitafunga,” alisema.

Nyota huyo amecheza mechi 10 kati ya 12 na kuyeyusha dakika 279 kwenye mechi za ligi.

KISA WAWA KUSOTA SANA BENCHI…WADAU WAPAZA SAUTI…WADAI AMERIDHIKA..APEWA ONYO KALI.. KOCHA WA LUIS MIQUISSONE AZIDI KUKAMUA MAMILIONI YA AL ALHY…ATAKA MKATABA WA ML 450 KWA MWEZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply