WINGA wa Yanga, Dickson Ambundo, amefunguka na kuelezea matumainiyake ndani ya kikosi hicho baada ya juzi Jumapili kufunga bao la ushindi dhidi ya Polisi Tanzania.
Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakikusanya alama 35, juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, iliibuka na ushindi wa bao 0-1 dhidi ya Polisi Tanzania.
Ambundo alifunga bao hilo dakika ya 64 akimalizia pasi ya Fiston Mayele. Hilo ni bao la kwanza kwa Ambundo tangu ajiunge na Yanga msimu huu akitokea Dodoma Jiji.
Akizungumza na Spoti Xtra Ambundo, amesema kuwa: “Nimejisikia furaha kufunga kwa mara ya kwanza kwenye
mchezo muhimu kama ule. “Malengo yangu ni kuhakikisha ninaisaidia timu kutwaa ubingwa, siwezi kusema nitafunga mabao mangapi, ila nitajitaidi kuhakikisha timu yangu ninaisaidia kuchukua ubingwa.
“Mashabiki wa Yanga wawe na imani na timu yao, Mungu akipenda tutabebea ubigwa msimu huu.”