Home news BAADA YA KUHAKIKISHA MUKOKO KASEPA JUMLA YANGA…NABI AIBUKA NA KUANIKA WAZI UBOVU...

BAADA YA KUHAKIKISHA MUKOKO KASEPA JUMLA YANGA…NABI AIBUKA NA KUANIKA WAZI UBOVU WAKE..


KIUNGO aliyetamba na Yanga, Mukoko Tonombe ‘Teacher’ ameshasepa zake kwenda TP Mazembe ya DR Congo iliyomsajili kwa mkataba wa miaka miwili, huku aliyekuwa kocha wake, Nasreddine Nabi akifichua kilichomponza Jangwani.

Mukoko aliyekuwa nahodha msaizidi wa Yanga ni kati ya wachezaji waliong’ara msimu uliopita kabla ya kupoteza namba baada ya maingizo mapya na uongozi kumpeleka Mazembe akipishana na Chico Ushindi.

Kabla ya kuondoka, Mukoko alidaiwa kugomea dili la kwenda Mazembe ili kumpisha Chico, kabla ya kueleweshwa na kuafikiana na mabosi wake akasaini mkataba mpya na wababe hao wa DR Congo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi amemtakia kila la heri kiungo huyo katika maisha yake mapya, lakini akifunguka kilichomfanya aruhusu aondoke kikosini, huku akiitaja Simba.

Nabi aliliambia gazeti la Mwanaspoti katika mahojiano maalum kwamba sababu kubwa iliyomfanya kumruhusu Mukoko kujiunga na Mazembe ni kutotunza ubora wake.

Alisema Mukoko alikuwa katika kiwango bora msimu uliopita, lakini baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba iliyopigwa Kigoma aliporomoka kiasi cha kushangaza. “Mukoko ni mtoto wangu wa kiume. Nafikiri mnajua jinsi tulivyokuwa na maisha mazuri wakati nafika hapa, lakini kuna mambo yalibadilika baada ya muda hapa lazima tuweke wazi,” alisema.

“Msimu huu ulipoanza hakuwa tena Mukoko yule licha ya kufanya juhudi kubwa kumrudisha katika ubora wake ule wa awali.”

Kocha huyo alisema Mukoko wa msimu huu aliangushwa zaidi na wenzake waliosajiliwa ambao walimzidi kiushindani katika kikosi hicho.

Alisema walifanya vikao mara kadhaa kumtaka kubadilika napia kumpa mbinu za kurejea katika ubora, lakini ilikuwa ngumu.

“Tulizungumza naye sana bahati nzuri makocha wote tumefanya naye kazi kabla ya msimu huu. Tulifanya kila tunaloweza kumrudisha lakini alishindwa kurudisha ubora wake kiushindani ndani ya timu,” alisema Nabi.

“Tukaona ni kama akili ya kutaka kuondoka inamzidi nguvu. Kuna wakati huwezi kuzuia sana hisia za mtu kama anafikiria kuondoka, kwa hiyo ilipokuja hii ofa hakukuwa na namna ya kuweza kuzuia hilo.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA MAKEKE YAKE...MORRISON AONGEZEWA 'SINDANO' YANGA....NABI AMPA UANGALIZI MAALUMU...

AMPA NAFASI MAZEMBE

Bosi wa Mazembe aliyesimamia usajili wa kiungo huyo, Andrea Mutini aliliambia Mwanaspoti kuwa, “Mukoko kama kushindwa ashindwe yeye, Mazembe tuna kocha mzungu (Franck Dumas), hata kabla ya kuzungumza na Mukoko na Yanga tulishamjulisha juu ya usajili huu na alimfuatilia na akakubali tumlete.”