Home news AFISA HABARI SIMBA AFUNGUKA ISHU YA YANGA KUMTAKA AENDE KWAO…AGUSI ISHU YA...

AFISA HABARI SIMBA AFUNGUKA ISHU YA YANGA KUMTAKA AENDE KWAO…AGUSI ISHU YA KUFUKUA MAFAILI…


OFISA Menaja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabu ya Yanga wanatamani kuwa na mtu kama yeye ndio maana alipochukuliwa na Simba wakaanza kufukua mafaili yake ikiwemo picha alizopiga na Yanga.

Ahmed amesema hayo leo, Jumatano, Januari 19, 2022 wakati akifanya mahojiano na Kituo cha Radio cha WASAFI FM jijini Dar es Salaam.

“Yanga wanatamani kuwa na mtu kama mimi, ndiyo maana baada ya uteuzi wangu wakawa wanahaha kuanza kutafuta mafaili kuonyesha kwamba huyo pia ni Yanga, hii ni ishara kwamba hata wao wanatamani kuwa na mtu kama mimi.

“Angeteuliwa hafisa habari wa kawaida kawaida pale simba, wasingehangaika kufukua mafaili, wasinge hangaika kutafuta taarifa zangu, lakini kwa kuwa nimeteuliwa mimi ambaye wananipenda, wananihitaji niwe pale kwao ndio maana wakaanza kuhangaika,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA UCHEZAJI WA 'SURE BOY' AKIWA YANGA..CHUJI AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here