Home news BAADA YA KUONA UCHEZAJI WA ‘SURE BOY’ AKIWA YANGA..CHUJI AGUNA KISHA AFUNGUKA...

BAADA YA KUONA UCHEZAJI WA ‘SURE BOY’ AKIWA YANGA..CHUJI AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA…

 


DAKIKA 90 za kwanza za kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ zilitosha kuthitibitisha kiungo huyo mpya wa Yanga bado ni yule yule hajapoa na sasa anaibua vita nyingine mpya kikosini.

Sure boy alicheza dakika 90 za kwanza ndani ya Yanga juzi usiku katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa Jang’ombe na hakika kuna kitu amekileta Jangwani na kuzidi kumpa ugumu Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Pasi 58 zimefika

Jamaa huyo ameonyesha mwendelezo wake wa ubora wa kupiga pasi kwani katika pambano hilo alipiga jumla ya pasi 59 na ni moja tu, iliyopotea, ila nyingine 58 zikifika kwa kiwango cha juu kwa wahusika.

Anakaba freshi tu

Ukiacha ubora wake wa kuchezesha timu hata akiwa anacheza kiungo cha chini lakini Sure boy ameonyesha pia ana msaada pale timu inapopoteza mpira hata kama akiwa juu anaanzia hukohuko kukaba mipira kisha kushuka chini zaidi kuongeza idadi ya wale wanaotakiwa kupokonya mipira.

Pasi za mwisho zipo

Katika mchezo huo dhidi ya Taifa Jang’ombe ambao Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 kama washambuliaji wa Yanga wangekuwa makini kulikuwa na pasi nne za mabao ambazo zilitoka katika mguu wa kulia wa Sure boy.

Hili ni kubwa na sasa kwa michezo ambayo ataichezea Yanga na kama akipewa nafasi ya kucheza kiungo mshambuliaji washambuliaji wa Yanga wanatakiwa kuwa makini kutumia pasi zake.

Kazi ipo na Aucho

Yanga sasa haina presha hata kama kiungo wao Khalid Aucho akikosekana, wana uhakika wanaye Sure boy anayejua kufanya kazi ya Mganda huyo vizuri, lakini kitu kibaya kwa wapinzani ni siku kocha wa Yanga Nesreddine Nabi awape nafasi wote, nafikiri kutakuwa na moto mkubwa zaidi kutokana na ubora wa watu wote hao katika kupiga pasi.

Msikie Chuji

Kiungo wa zamani wa Yanga na Simba, Athuman Idd ‘Chuji’ alisema Sure boy ameonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa juzi na kazi kubwa sasa aliyonayo ni kuwa na muendelezo bora wa kiwango chake.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KUFUZU CHAN.....'VIBE' LA TAIFA STARS LAMKUNA KIM POULSEN...AWAANDALIA SOMALIA 'KARAMU'...

Chuji alisema Sure boy ataisaidia Yanga kutokana na aina ya pasi zake ambapop sasa anaonekana kukomaa zaidi akiwa na pasi za kwenda kutafuta ushindi.

“Sure Boy nimemwona nafikiri bado yuko katika ubora mkubwa uleule ambao tunaujua lakini sasa anapiga sana pasi za kwenda mbele viungo wetu wengi wanakosa ubora huu,” alisema Chuji.

“Kitu kingine ameonyesha anaweza kuzalisha pasi za mwisho huu ni kama mtaji mkubwa kwa timu na uzuri Yanga wana vijana sasa ambao wanakimbia nafikiri changamoto kubw kwake sasa ni kuwa na mwendelezo wa kiwango chake.

“Kuhusu kupata nafasi katika kikosi cha Yanga kocha wake ataamua kulingana na mchezo wanaocheza unapokuwa na Sure Boy na Aucho hawa watu wote wana ubora na uzoefu mkubwa.”

Kocha Cedric Kaze amesifia kiwango kizuri cha Sure Boy kwenye mchezo huo akisema yeye na Denis Nkane wameonyesha kuingia kwenye mfumo wake, licha ya ugeni wao kikosini.