Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA COSTAL….YANGA YA GSM WAPANGA KUUWASHA MOTO..YAZANZIBAR BADO YAPO…

KUELEKEA MECHI DHIDI YA COSTAL….YANGA YA GSM WAPANGA KUUWASHA MOTO..YAZANZIBAR BADO YAPO…


KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Kikosi cha Yanga kimerejea kambini jana Jumatano ambapo uongozi umefunguka kuwa utaenda kucheza mchezo huo wakiwa na kikosi kamili ili kujihakikishia ubingwa.

Yanga ilirejea Dar juzi Jumanne ikitokea Zanzibar baada ya kutolewa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC.

Akizungumza na Gazeti la Spoti Xtra, Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro, alisema kuwa: “Tunamshukuru Mungu timu imerejea salama kutoka Zanzibar na imeanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu kwa upande wetu, lakini tunajipanga kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwani kilichotokea Zanzibar ilikuwa bahati mbaya.

“Baada ya likizo ya muda mfupi ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi amesharejea nchini toka juzina kikosi kitaondoka Dar Ijumaa (leo) kuelekea Tanga kwenye mchezo huo.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA KILELENI...UONGOZI YANGA WAIBUKA A HILI JIPYA..WAIBANA SIMBA KISAWASAWA...