Home news SIKU CHACHE BAADA YA KUKARIBISHWA YANGA…MBRAZILI WA MAKIPA ATOA ‘KOMENTI’ HII KWA...

SIKU CHACHE BAADA YA KUKARIBISHWA YANGA…MBRAZILI WA MAKIPA ATOA ‘KOMENTI’ HII KWA MSHERY…


KOCHA mpya wa makipa wa Yanga, Mbrazili, Milton Nienov amefunguka kuwa usajili wa kipa, Aboutwalib

Mshery ni usajili bora kufanywa na klabu hiyo kutokana na ubora wake, huku akiweka wazi kuwa ameanza na suala la kuhakikisha makipa wa timu hiyo wanahimili presha ya michezo mikubwa.

Milton alitambulishwa rasmi na Yanga Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo alikuwa sehemu ya mashuhuda wa mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga huku Yanga wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kabla ya kujiunga na Yanga, Milton alikuwa akihudumu kama kocha wa makipa wa Simba kabla ya kuachana nao Oktoba 26, mwaka jana muda mfupi baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Championi Jumatano, kuhusu kiwango cha makipa wa timu hiyo, Milton alisema: “Siwezi kuzungumza mengi kuhusiana na uwezo wa makipa wetu kwa sasa, kwa kuwa ndiyo kwanza nimefika hapa lakini katika vipindi vichache vya mazoezi ambavyo nimekuwa pamoja nao naweza kusema tuna makipa bora sana.

“Huyu Mshery ni kijana mdogo na mwenye uwezo mkubwa sana, naamini ulikuwa usajili bora kwetu,niliona alikuwa na presha kidogo kwenye mchezo dhidi ya Coastal na nimepanga kuhakikisha nalifanyia kazi hilo kwa kuwa ni muhimu kwa kipa kuhimili presha ya michezo mikubwa ili kutofanya makosa.”

SOMA NA HII  KAZADI AMTAJA NYOTA ALIYEMSHAWISHI KUJIUNGA YANGA