Home news UKWASI WA MO DEWJI NI BALAA…ANAWEZA KUJENGA UWANJA NA KUINUNUA YANGA YOTE...

UKWASI WA MO DEWJI NI BALAA…ANAWEZA KUJENGA UWANJA NA KUINUNUA YANGA YOTE NA CHENJI IKABAKI…


WAKATI mashabiki wa Simba wakisumbuliwa na msongo wa mawazo kutokana na matokeo mabaya waliyopata hivi karibuni Rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ametajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 18 wa Afrika kwa ripoti ya mwaka 2022.

Katika orodha hiyo ya jarida la Forbes kwa mwaka huu limemtaja MO kuwa bilionea namba 15 akifungana na matajiri wengine wawili Othman Benjelloun na Youssef Mansour wote wakiwa na utajili sawa.

Utajiri wa Mo umetajwa kufikia Dola bilioni 1.5 (Sh3.4 trilioni) utajiri ambao ni sawa na mwaka jana hivyo hajaongeza wala kupunguza.

Aidha kwa utajiri huo, Mo akiamua kuwekeza zaidi kwenye timu yake anaweza kusajili mchezaji yeyote yule Afrika, pamoja na kujenga miundombinu ya Simba, ikiwemo uwanja ambao imetajwa kuwa unaweza kugharibu bilioni thelathini.

Pia kama akiamua kuonyesha jeuri ya pesa, Mo dewji anaweza kusajili wachezaji wote wa Yanga pamoja na kocha wake , na akabakiwa na chenji ya kutosha.

Katika orodha ya jarida hilo mwaka jana Mo ambaye ni raia wa Tanzania anayefanya biashara mchanganyiko alikuwa nafasi ya 15 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.5 (3.4 trilioni).

Uwekezaji katika viwanda vya nguo, unga wa ngano na sembe, mafuta ya kupikia, sabuni, sukari na vinywaji unatajwa kama chanzo cha utajiri huo wa Dewji ambaye kwa hapa Tanzania yeye pekee ndiye ameingia katika orodha hiyo ya mataikuni 18 barani Afrika.

Kwa kuingia katika orodha hiyo, Dewji anafuata nyayo za Mmiliki wa Mamelodi Sundowns, Patrice Motsepe amabye yeye ana utajiri unakadiriwa kufikia Dola 3 bilioni (zaidi ya Sh 9 trilioni)

Pia Dewji ndiye mtu pekee kutoka Afrika Mashariki aliyeweza kuingia katika orodha hiyo kwa mujibu wa Forbes huku nchi za Afrika Kusini, Nigeria na Misri zikitawala.

Aliko Dangote aliyewekeza katika biashara za sukari na simenti anashika nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa Dola 13.9 bilioni na anafuatiwa na Johann Rupert & family mwenye utajiri wa Dola 11 bilioni huku nafasi ya tatu ikishikilia na Nicky Oppenheimer wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 8.7 bilioni.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHINDA MECHI YAKE YA KWANZA KAMA KOCHA MKUU SIMBA....MATOLA FUNGUKA ALICHOKIFANYA NYUMA YA PAZIA...