Home news WAKATI SIMBA WAKICHEZA LEO…PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA YOTE YANAYOENDELEA NDANI…

WAKATI SIMBA WAKICHEZA LEO…PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA YOTE YANAYOENDELEA NDANI…


KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, juzi Alhamisi alishuka na kikosi cha klabu hiyo kutokea mkoani Kagera, na kuchimba mkwara mzito kuwa wamesahau kuhusu matokeo yao mabaya kwenye michezo iliyopita na wamekuja kuanza vita mpya.

Simba Januari 26, 2022 walipata kipigo dhidi ya Kagera, Kaitaba. Baada ya kurejea Dar, Simba sasa wanajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), dhidi ya Dar City leo Jumapili kwa Mkapa.

Kocha Pablo alisema: “Kwanza kabisa niweke wazi kuwa kama kikosi tumesikitishwa na matokeo ambayo tumeyapata katika michezo yetu mitatu iliyopita, kama utaniuliza mimi ningekwambia hatukustahili kupata matokeo yale kutokana na nafasi ambazo tulitengeneza lakini wakati mwingine hivyo ndivyo mpira ulivyo.

“Tunatarajia kuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Dar City, haya ni mashindano mengine ambayo tunatetea ubingwa wake hivyo tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ili kurejesha hali ya kujiamini, tutapambana kama fainali kwa kila mchezo ulio mbele yetu na naamini tuna nafasi ya kufanya vizuri.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA YANGA IKICHEZA JUZI..ZAHERA AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA...