Home news WAKATI SIMBA WAKIWA ‘BIZE’ NA CHEREKO…YANGA WASHUSHA JEMBE JIPYA KIMYA KIMYA…KAMA UTANI...

WAKATI SIMBA WAKIWA ‘BIZE’ NA CHEREKO…YANGA WASHUSHA JEMBE JIPYA KIMYA KIMYA…KAMA UTANI VILE…


Wakati Simba jana wakiwa ‘bize’ na kutua kwa Chama, Yanga kimya kimya walimtambulisha Beki wa Kati kutoka KMKM ya Zanzibar Ibrahim Bacca.

Ibrahim ambaye aling’ara kwenye michuano ya Mapinduzi iliyoisha juzi Jumatano , anaendaYanga kuongeza idadi ya mabeki wa kati watakao wania nafasi ya kwanza kwenye kikosi hiko, ambapo mpaka sasa atakuwa na ushindani wa namba na mabeki wazoefu kama Mwamnyeto, Job, Ninja na wengineo.

๐—œ๐—•๐—ฅ๐—”๐—›๐—œ๐—  ๐—•๐—”๐—–๐—–๐—” is Green & Yellow๐Ÿ”ฐ#TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko pic.twitter.com/coQMPrlQwQ

โ€” Young Africans SC (@yangasc1935) January 14, 2022


Hata hivyo inafahamika kuwa Ibrahim amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ,ambapo kama atakuwa na kiwango kizuri cha kumshawishi Nabi huenda akaongezewa zaidi.

Huu unakuwa ni usajili wa nne kwa Yanga kwa wachezaji wa ndani kwenye dirisha hili dogo la usajili, Wengine waliosajiliwa hivi karibuni ni pamoja na Golikipa Mshery, Kiungo Denis Nkane, pamoja na mshambuliaji Chrispin Ngushi kutoka Mbeya Kwanza pamoja na Sure Boy kutoka Azam FC.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONYESHA KIWANGO CHA 'DUNIA'...KOCHA MSAUZI AIBUKA NA HILI KWA SALIM ALLY...