WAKATI mashabiki wa Simba wakiendelea kuamini kuwa, hata msimu huu chama lao litapindua matokeo mwishoni na kutetea tena mataji yao, mabosi wa Simba wamecheka sana na kuwaambia; ‘Msijidanganye, sisi hatuachi kitu’.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa katika mahojiano maalumu na kusema baada ya kupoteza taji lao la michuano ya Kombe la Mapinduzi, hawataki tena kupoteza malengo yao muhimu.
Senzo alisema malengo yao makubwa wamejiwekea ni kuchukua Kombe la Ligi na lile la Shirikisho (ASFC) na kusisitiza wamweka mkazo kwa kila mechi.
“Mapinduzi ilishapita na sasa tunaendelea kusonga mbele zaidi, tunafanya kazi kubwa sio tu kwa wachezaji bali kila mtu katika timu hii na lengo likiwa ni kuchukua mataji, hatutaki kuacha kitu tena,” alisema Senzo na kuongeza:
“Tunajua kila timu katika ligi na hata kwenye ASFC ni kutamani kuwa bingwa, lakini sisi tuna kiu zaidi na kumejipanga mapema kufanikisha hilo, hivyo wale wanaoamini watapindua meza jioni, imekula kwao, Yanga ya sasa ipo kivingine.”
Senzo alisea kutika kuthibitisha kuwa Yanga imejipanga ni kuangalia aina ya usajili iliyofanya safari hii kwa kubeba wachezaji wenye ubora na uwezo wa kuipambania timu kwa kila mechi na imeonekana katika Ligi Kuu na ASFC.