News

KISA CHAMA NA BWALYA…PABLO ATIKISA KICHWA KISHA ANENA HAYA…ATANGAZA HATARI…

admin February 3, 2022 5:00 am


UWEZO mkubwa ambao umeonyeshwa na kikosi cha Simba hususani viungo wao raia wa Zambia, Clatous Chama na Rally Bwalya kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi Dar City umemuibua kocha mkuu, Pablo Franco ambaye ameweka wazi kuwa hawatakata tamaa kuhusu ubingwa wao na watapambana kushinda kila mchezo ulio mbele yao.

Simba Januari 30, mwaka huu wakiwa katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dar City katika mchezo wa hatua ya 32 ya michuano ya Kombe la Shirikisho laAzam ambapo walifanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora huku Chama na Bwalya wakionyesha uwezo mkubwa.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Simba katika michezo yao minne mfululizo iliyopita ambapo michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara walipoteza michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja.

Akizungumza hivi karibuni, Kocha Pablo alisema: “Ni jambo zuri kuweza kupata ushindi huu muhimu dhidi ya Dar City, hususani baada ya kupitia kipindi kigumu cha kukosa matokeo katika michezo mitatu mfululizo ya ligi kuu.

“Lakini kama ambavyo nilieleza hapo awali, kwetu yaliyopita yamepita na tunawekeza katika michezo yetu ijayo, hatukati tamaa kwa kuwa hakuna anayeweza kutabiri nini kitatokea mwishoni mwa msimu, hivyo la muhimu kwetu ni kushikamana na naamini tutajitahidi kushinda kila mchezo ujao.”

CHAMA AKABIDHIWA ZIGO LA LAWAMA SIMBA…PABLO AFANYA UMAFIA CAF..JEURI YA UBINGWA YANGA IPO HAPA… PAMOJA NA SIMBA KUPITWA NA YANGA KWA POINT 10…PABLO AVUNJA UKIMYA …ATOA KAULI HII…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply