news

MIEZI KADHAA TANGU ATUE MOROCCO…KISINDA NAYE AANZA YA CHAMA…ATUMA UJUMBE HUU YANGA…

admin February 4, 2022 2:26 pm


ALIYEKUWA winga wa Yanga, Tuisila Kisinda, amefunguka kufurahishwa na klabu yake ya zamani kuongoza ligi kwa alama nyingi dhidi ya Simba huku akiweka wazi kuwa matamanio yake ni kuiona Yanga ikitwaa ubingwa msimu huu.

Kisinda ambaye amedumu kwa msimu mmoja pekee ndani ya Yanga, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco inayonolewa na kocha Florent Ibenge.

Akizungumza na gazeti la Championi Ijumaa, Kisinda alisema kuwa anajisikia furaha kuona timu yake ya awali ikiwa inafanya vizuri katika msimamo wa ligi kuu huku akiweka wazi kuwa anatamani kuona timu hiyo ikitwaa ubingwa msimu huu mara baada ya msimu uliopita kuukosa.

“Nafurahi kuiona Yanga ikiwa inaongoza mbele ya Simba tena kwa pointi nyingi, msimu uliopita ubingwa haukuwa kwa Yanga lakini kwa hiki ambacho kinaendelea kwa sasa ni dalili nzuri za ubingwa.

“Mimi napenda kuiona Yanga ikifanikiwa mara baada ya kushindwa kutwaa kwa muda mrefu ubingwa wa ligi kuu, hivyo nitafurahi kama ndoto hizo zitakamilika kwa Wanayanga kufurahia ubingwa wao,” alisema mshambuliaji huyo.

EHEE..KUMBE KIWANGO KIBOVU CHA CHIKO USHINDI SABABU NI HII TU?…NABI AVUNJA UKIMYA…. BAADA YA KUSHINDWA KUFURUKUTA CAMEROON NA TIMU YA TAIFA…PRINCE DUBE AIBUKA NA HILI KWA AZAM…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply