Home news HIZI HAPA SABABU ZA NDANI KABISA ZA GSM KUJITOA UDHAMINI WA LIGI...

HIZI HAPA SABABU ZA NDANI KABISA ZA GSM KUJITOA UDHAMINI WA LIGI KUU…GHARIB KASUSA MPAKA….


KAMPUNI ya GSM imejiondoa kama mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara baada ya mkataba wao kutokwenda kama walivyotarajia.

Ofisa Biashara wa GSM,  Allan Chonjo amesema wamejiondoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu baada ya TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kusimamia matakwa yaliyopo kwenye mkataba walioingia.

Akizungumza na wanahabari leo katika makao makuu ya GSM yaliyopo Posta, Chonjo amesema waliwaandikia barua TFF  baada ya kuona tofauti na ilivyo kwenye mkataba.

“Haya hayajawa maamuzi rahisi kwa kampuni ya GSM kwani tunatambua vipo baadhi ya klabu za mpira zitaumizwa pamoja na  wadau mbalimbali na hatua hii haikuwa dhamira yetu kufikia uamuzi huu mgumu,” amesema Chonjo na kuongeza;

 “Upandewa klabu udhamini wa klabu tutaendelea kuwa kwenye mkataba wetu kama kawaida bali tumejitoa upande huu wa Ligi.”

Wakati huohuo Chonjo alisema;”Ghalib Said amejiondoa kwenye kamati ya Uenyekiti wa kamati ya ushindi ya timu ya Taifa Tanzania pamoja na nafasi ya ujumbe”.

Mkataba wa GSM na TFF ulisainiwa Novemba mwaka jana hivyo umedumu kwa siku 76 tu.

Kampuni wa GSM, iliingia mkataba wa miaka miwili na Ligi Kuu Bara wenye thamani ya Sh2.1 Bilioni kama mdhamini mwenza.

SOMA NA HII  LIGI YA WANAWAKE IMEKAMILIKA, ZAWADI ZAO WAPEWE KWA WAKATI