Home news WAKATI CHAMA AKIIRUDISHA SIMBA KWENYE SAYARI YAKE…BOCCO MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU..UKWELI UKO...

WAKATI CHAMA AKIIRUDISHA SIMBA KWENYE SAYARI YAKE…BOCCO MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU..UKWELI UKO HIVI..


DAKIKA 90, zimemalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Mbeya Kwanza.

Bao la Simba limewekwa kimiani na kiungo wake Clatous Chama dakika ya 80, baada ya kutokea sintofahamu kwenye eneo la ulinzi kufuatia mabeki wa Mbeya Kwanza kudhani nyota na mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere kaotea.

Mabadiliko ya kuwatoa Jonas Mkude na John Bocco yalionekana kuleta tija kwa upande wa wenyeji ambao walikuwa na wakati mgumu kwa muda mrefu wa kupenya safu ya ulinzi ya Mbeya Kwanza.

Mbeya Kwanza iliendelea kuwa na mikakati mizuri ya kuwaheshimu wapinzani wao kwani kwa muda mwingi walionekana kushambulia na kuzuia kwa pamoja licha ya kushindwa kuhimili presha ya mashambulizi iliyokuwa inaelekezwa langoni mwao.

Bao la Chama ni la kwanza kwa Simba msimu huu katika Ligi Kuu Bara tangu asajiliwe katika dirisha dogo la usajili akitokea RS Berkane ya Morocco.

Ushindi huu unakuwa muhimu kwa Simba kwani katika michezo 15, iliyocheza imekusanya pointi 31, nyuma ya pointi tano tu na vinara Yanga yenye 36, ingawa wana mchezo mmoja mbele.

Kwa upande wa Mbeya Kwanza inaendeleza jinamizi la kutoshinda michezo ya Ligi Kuu Bara tangu mwaka huu kuingia ambapo kwa matokeo haya yanaifanya kusalia na pointi 13 ikiwa nafasi ya 12.

SOMA NA HII  KISA 'MAVITUZI' YA SAKHO....WASUDANI WAIWEKEA SIMBA MEZANI BILIONI 1.3...VIONGOZI WAJING'ATA NG'ATA...