Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara wamepigwa faini ya Sh500,000 kila mmoja na kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi imesema walifanya kosa la kuwashutumu waamuzi wa Ligi Kuu Bara kupitia mkutano wa waandishi wa habari.
“Manara na Bumbuli walizungumza na wanahabari Februari 8 kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu hiyo ambapo walishutumu waamuzi wa ligi kuu kwa masuala mbalimbali waliyoyausisha na upendeleo,” imeeleza taarifa hiyo
TPLB imesema kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mpira wa miguu mtunza muda katika mechi ni mwamuzi pekee.
“Kamati imetoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kuhoji suala la muda wa nyongeza katika mechi za Ligi,”