Home news A-Z JINSI SIMBA ‘ILIVYOWASOSOMOLA YANGA’ WA IVORY COST …BANDA, SAKHO WAAANZA...

A-Z JINSI SIMBA ‘ILIVYOWASOSOMOLA YANGA’ WA IVORY COST …BANDA, SAKHO WAAANZA KULIPA MSIMBAZI….

 


DAKIKA 90, zilikamilika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Asec Mimosas katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Mabao ya Simba yamewekwa wavuni na Pape Sakho, katika kipindi cha kwanza na mengine yakiwekwa nyavuni kipindi cha pili na Shomari Kapombe kwa mkwaju wa penalti na winga Peter Banda.

Kwa upande wa Ases Mimosas ilianza vyema kipindi cha pili huku ikionekana kushambulia tofauti na kipindi cha kwanza na dakika ya 59, ilijipatia bao la kusawazisha kupitia Kwa Aziz Stephane kufuatia uzembe uliofanyika katika eneo la ulinzi.

Dakika ya 75, Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Meddie Kagere, Sadio Kanoute huku nafasi zao zikichukuliwa na John Bocco na Yusuph Mhilu Ili kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji ambalo lilionekana kupoa zaidi kipindi cha pili.

Mabadiliko hayo yalileta tija kwani dakika ya 79, Simba ilipata bao la pili kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa beki Shomari Kapombe baada ya kipa wa Ases Mimosas Abdoul  Cisse kumfanyia madhambi Yusuph Mhilu katika eneo la hatari.

Wakati Asec Mimosas ikiendelea kujiuliza jinsi ya kurejesha bao hilo Simba ilifanya shambulio la kushtukiza na kujipata bao la tatu kupitia kwa winga wake Mmalawi Peter Banda na kuanza vyema michuano hii hatua ya makundi.

Baada ya mchezo huu Simba itashuka Uwanja ni Februari 15, kupambana na Ruvu Shooting

kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hatua ya 16 bora kisha kuelekea ugenini katika michezo miwili ya kimataifa dhidi ya US Gendarmerie Nationale ya Niger Februari 20, na RS Berkane ya Morocco Februari 27.

SOMA NA HII  YANGA SC:- FEI TOTO AMEVUNJA KANUNI...TULITAKA KUMPA MKATABA MPYA ....