news

KISA USHINDI WA JANA DHIDI YA BIASHARA…MWAMNYETO AVUNJA UKIMYA YANGA..AWATAJA MASHABIKI …

admin February 16, 2022 9:09 am

 


Baada ya kuibamiza Biashara United Mara mabao 2-1 na kuitupa nje ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, Nahodha na Beki wa Young Africans Bakari Nondo Mwamnyeto ametoa neno la kishujaa.

Young Africans iliipa kisago Biashara United Mara jana Jumanne (Februari 15), Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, na kutinga hatua ya Robo Fainali.

Mwamnyeto amesema msimu huu wamejipanga kupambana na kufikia lengo la kutwaa ubingwa wa Michuano hiyo ‘ASFC’ na Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo ‘Aliye Mbele Yao Ajipange.’

Amewataka mashabiki wa Young Africans kuendelea kukiamini kikosi chao, na kufika Uwanjani kwa ajili ya kuwapa nguvu wachezaji, ambao wanapambana kwa ajili yao, ili kufikia lengo la kuwa Mabingwa.

“Aliye mbele yetu ajipange, Mipango yetu msimu huu ni kutwaa Ubingwa. Tunaomba mashabiki waendelee kuja kwa wingi Uwanjani, Sisi ni timu yao na tunashinda kwa ajili yao.” Amesema Bakari Mwamnyeto.

Mbali na kutangulia Robo Fainali ya ‘ASFC’ Young Africans inaongoza Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 36 ikicheza michezo 14, huku Mabingwa watetezi Simba SC wakiwa nafasi ya pili kwa kufikisha alama 31 baada ya kucheza michezo 15.

BAADA YA KUONA PIRA LA  SIMBA JUZI…MASAU BWIRE AGUNA KISHA AKASEMA HILI KUHUSU MECHI YA LEO… INONGA AFUNGUKA ALIVYOWAKIMBIA YANGA…AGUSIA ALIYEMTONYA KUHUSU RAHA ZA SIMBA…MUKOKO ATAJWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply