News

BAADA YA SIMBA KAMPIGA MTU SABA….MWAMNYETO AKUNA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA HAYA KUHUSU YANGA…

admin February 18, 2022 2:17 pm


BEKI wa kati wa Yanga ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto, amesema safari hii wanahitaji kufika fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kuwa mabingwa.

Yanga juzi Jumanne walifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mwamnyeto alisema, malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa michuano hiyo.

“Tunatakiwa kufika fainali ili tuwe mabingwa wa a michuano hii, akili zetu na malengo yetu yapo katika michuano hii na lazima tuhakikishe tunatimiza.

“Wapinzani wanatakiwa kujipanga kwani hata sisi tayari tumeshajipanga kucheza na timu yoyote itakayojitokeza mbele yetu, hakuna jambo ambalo lisilowezekana, ni kujituma tu na kuwa na nia ya kuwa mabingwa na sisi tunayo nia,” alisema nahodha huyo.

KIFAA CHA MAZEMBE CHAKUTANA NA ‘NKONO WA NTU’ YANGA….AUMWA GHAFLA…ACHUJWA RASMI… YANGA WAFANYA KWELI BUNGENI…WAIPIGA BAO SIMBA …WAMBEBA JUMLA JUMLA SPIKA TULIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply