News

YANGA WAFANYA KWELI BUNGENI…WAIPIGA BAO SIMBA …WAMBEBA JUMLA JUMLA SPIKA TULIA…

admin February 18, 2022 2:35 pm


KLABU ya Yanga leo Februari 18 imefanya uzinduzi wa kadi mpya za Uanachama za kielektroniki kwa Wabunge wa Bunge Ia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wanachama wa Yanga.

Uzinduzi wa kadi za kielektroniki ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko ya kidigitali na ya mfumo wa uendeshaji wa klabu kwa mujibu wa katiba ya Yanga toleo Ia 2021.

Hafla ya uzinduzi huo umefanyika kwenye Hoteli ya Morena jijini Dodoma kuanzia saa 4:00 asubuhi ambapo mgeni rasmi alikuwa Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson ambapo alikabidhiwa kadi mpya ya uanachama.

Itakumbukwa pia, Spika Dk Tulia ni mwanachama na mshabiki kindakindaki wa Simba SC, ambapo mara kadhaa huyaweka mahaba yake kwa Simba SC hadharani.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Wabunge, Viongozi wa Klabu ya Yanga, wadau na waandishi wa habari.

BAADA YA SIMBA KAMPIGA MTU SABA….MWAMNYETO AKUNA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA HAYA KUHUSU YANGA… KUHUSU KUCHEZA NA YANGA MANUNGU….MTIBWA WAIBUKA NA HILI… THOBIAS KIFARU AITAJA TABORA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply