news

KUELEKEA MECHI YA JUMAPILI…MKUDE AMUWAHI MUARABU…MWENDA NAYE ARUDI…

admin February 25, 2022 4:50 pm


SIMBA jana ilitua Casablanca tayari kwa safari ya kuifuata RS Berkane mjini Berkane kwa mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku nyota wao, Jonas Mkude na Israel Mwenda wakirejea mapema kuwawahi Wamorocco hao.

Wachezaji hao walishindwa kucheza mchezo uliopita wa Kundi D dhidi ya USGN ya Niger ulioisha kwa sare ya 1-1 baada ya kuugua ghafla, lakini kwa sasa wamepona na wameanza kujifua na wenzao.

Kuumwa kwa Mkude kulifanya akosekane kabisa hata katika benchi, huku Mwenda alikaa tu kwa vile kulikuwa na idadi ndogo ya wachezaji wa akiba na Kocha Pablo Franco alisema ilikuwa ngumu kwenye maandalizi ya mchezo huo ikiwemo kuwakosa wachezaji wake kutokana na kuumwa.

“Ukiangalia katika benchi la akiba kulikuwa na makipa wawili, Ally Salim na Benno Kakolanya, jambo ambalo hata Mwenda alikaa kutimiza idadi ya wachezaji ila hakuwa fiti asilimia zote,” alisema Pablo.

Hata hivyo, Daktari wa Simba, Edwin Kagabo alisema baada ya kuwapatia matibabu wachezaji hao wanaendelea vizuri na baada ya kufika Morocco watafanya mazoezi pamoja na wenzao.

“Mkude na Mwenda wote wapo sawa kiafya tofauti na ilivyokuwa siku moja kabla ya kucheza na USGN, kuhusu kama watatumika kwenye mechi ya RS Berkane hilo ni la kocha lakini wapo fiti sasa,” alisema Edwin.

TFF YAWAPIGIA MAGOTI GSM…WARUDI MEZANI UPYA KUJADILI DILI..MGUTO ATUPA MPIRA KWA KIDAO.. KISA SIMBA…NABI ABADILI SILAHA ZA MAANGAMIZI YANGA…SIMBA  YAWAINGIZA CHAKA WAARABU..MORRISON AFICHWA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply