Home BIashara United KUELEKEA MECHI YAO DHIDI YA YANGA LEO..BIASHARA WAJITUTUMUA NA KUSEMA HILI…WAITAJA CAF….

KUELEKEA MECHI YAO DHIDI YA YANGA LEO..BIASHARA WAJITUTUMUA NA KUSEMA HILI…WAITAJA CAF….


KOCHA Mkuu wa Biashara United ya Mara, Vibier Bahati ameweka wazi kuwa watacheza kwa kufa na kupona kwenye mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwa ajili ya kupata matokeo.

Biashara watakuwa ugenini kwenye mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar Februari 15.

“Tangu msimu huu wa ligi uanze Yanga wamekuwa na timu bora yenye wachezaji wazuri, lakini sisi hatutaangalia hilo na badala yake tutapigana kufa na kupona ili tupate matokeo katika mchezo huo.

“Bado malengo yetu ni kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa CAF kwa hivyo dhamira yetu ni kutwaa ubingwa wa kombe hili ili hapo baadae tuwakilishe nchi kimataifa baada ya kufanya hivyo msimu huu japokuwa hatukuwa mabingwa wa mashindano haya.

“Tutautumia mchezo huo kujijenga uwanjani lakini pia kuangalia makosa ambayo tumeyarekebisha kama tumefanikiwa, tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kutuunga mkono,” alimaliza Bahati.

SOMA NA HII  WAKATI WATU WAKIDHANI WAKO 'SIRIAZI' NA UBINGWA WA LIGI TU....NABI AWASHANGAA WEE...KISHA AKASEMA HAYA..