Home news KUHUSU SIMBA KUBEBA UBINGWA MSIMU HUU…YANGA WAMPA ‘WAZIMU’ PABLO…AWAOMBEA ‘DUA LA MWEWE’…

KUHUSU SIMBA KUBEBA UBINGWA MSIMU HUU…YANGA WAMPA ‘WAZIMU’ PABLO…AWAOMBEA ‘DUA LA MWEWE’…


KOCHA Mkuu wa Simba, Muhispania, Pablo Franco amesema kwa ubora wa kikosi chake cha hivi sasa anapata matumaini makubwa ya kuipa timu hiyo ubingwa wa tano mfululizo wa Ligi Kuu Bara.

Jeuri ya kocha huyo anaipata kutokana na ubora na viwango vikubwa walivyokuwa nayo hivi sasa viungo washambuliaji wake ambao baadhi waliokuwepo katika kiwango bora ni Clatous Chama, Peter Banda, Pape Sakho na Rally Bwalya.

Simba iliyokuwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 37, inapambana hivi sasa katika msimamo wa ligi kwa ajili ya kuwaondoa Yanga wenye 45 kileleni.

Pablo alisema kuwa kwa jinsi vijana wake wanavyocheza soka safi la kuvutia huku wakifuata maelekezo yake, haoni sababu ya kushindwa kuutetea ubingwa huo wa ligi.

Pablo alisema kuwa anaamini uwezo wa kila mchezaji wake, licha ya kutofanya vizuri katika michezo ya mzunguko wa kwanza wa ligi kwa kufungwa dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar zote wakifungwa bao 1-0.

Aliongeza kuwa kwa upande na kushirikiana na wachezaji wake wamejipanga kushinda michezo yote 15 ya ligi huku akiamini wapinzani wao Yanga kupoteza katika michezo ijayo na kukaa timu hiyo.

“Ni mapema kukata tamaa ya ubingwa wa ligi, kwa jinsi msimu huu ulivyokuwa naamini inawezekana kwetu kuchukua ubingwa kwa mara ya tano mfululizo, licha ya kuwa nyuma kwa pointi kadhaa.

“Kikubwa ninawaamini wachezaji wangu, kama ambavyo tulishindwa kufanya vizuri katika baadhi ya mechi na kuachwa pointi hizo, wapinzani wetu nao linaweza kuwatokea jambo kama hilo.

“Niwaombe viongozi na mashabiki kuendelea kuwasapoti wachezaji wangu wanaoipambania timu yao uwanjani ili waipatie pointi tatu timu yao. Baada ya kutoka katika ligi sasa nguvu nazielekeza katika shirikisho,” alisema Pablo.

SOMA NA HII  USAJILI WA SIMBA WASHTUA...KOCHA MPYA ASHIKILIA MAFAILI YA MASTAA HAWA