Home news CHICO NA AUACHO WARUDISHA TABASAMU KWA NABI…NTIBAZONKIZA NA WENZAKE WAMPA PRESHA…

CHICO NA AUACHO WARUDISHA TABASAMU KWA NABI…NTIBAZONKIZA NA WENZAKE WAMPA PRESHA…


PAMBANO la Yanga na KMC limepigwa kalenda hadi Machi 19, lakini hiyo imekuwa nafuu kwa Kocha Nasreddine Nabi aliyekuwa na majeruhi wengi kikosini, huku baadhi ya nyota hao wakianza kurejea na kupunmguza presha Jangwani.

Awali mchezo huo wa Ligi Kuu ulipangwa upigwe Jumatano ijayo, lakini  Bodi ya Ligi ilitoa taarifa ya kuahirishwa sambamba na ule wa Simba dhidi ya Polisi Tanzania uliokuwa upigwe Machi 27, mjini Moshi ili kupisha mechi ya timu ya taifa kwa kalenda ya FIFA, japo timu haijafahamika.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya kuahirishwa kwa mchezo huo, umekuwa nafuu kwa Nabi, aliyeshusha pumzi baada ya baadhi ya mastaa wake kuanza kurejea kutoka katika majeruhi na ugonjwa akisema hali hiyo itawapa ari mpya ya kiuwania ubingwa.

Nabi alisema kuwa, baada ya mazoezi ya juzi waliporejea kazini ripoti ya madaktari inaonyesha wachezaji wasiopungua wanne wamerejea kazini.

Yanga juzi ilianzia gym mara baada ya kutoka mapumziko ya siku mbili ikitoka kuichapa Geita Gold kwa bao 1-0 kwenye mechi iliyopigwa, jijini Mwanza wikiendi iliyopita na kwa mujibu wa Nabi amepokea ripoti ya kurejea kwa Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Khalid Aucho, Farid Mussa na Chico Ushindi, jambo ambalo kwake ni faraja kubwa.

Kikosi hicho kiliingia kambini jana kujiandaa na mchezo huo na KMC, ikiwa na kumbukumbu ya kushinda 2-0 katika mchezo wa awali mjini Songea.

“Kurejea kwao ni nafuu, naamini wengine watarejea zaidi kama mambo yataenda kama nilivyoambiwa na madaktari,” alisema Nabi.

Katika dhidi ya Geita, Yanga iliwakosa Aucho, Jesus Moloko, Ninja, Saido Ntibazonkiza, Yacouba Songne, David Bryson na Farid Mussa waliokuwa majeruhi na Djuma Shaban na Chico waliokuwa wakiugua.

SOMA NA HII  SIMBA, YANGA ZAGOMBEA SAINI YA KIPA HUYU MZAWA