Habari za michezo

KISA SHEREHE YA NGUVU KWAO BURUNDI..SAIDO KUIKOSA MECHI YA YANGA vs KMC…MWALIKO WATOKA…

admin March 17, 2022 3:00 pm


NYOTA wa Yanga, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ anatarajia kufunga ndoa Jumamosi, Machi 19 na mpenzi wake Uwera Samantha ‘Samira’.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari  na mitandao ya kijamii nchini Burundi ndoa hiyo itafanyika kwa taratibu za dini ya kiislamu na baadae sherehe zitaendelea kwenye ukumbi wa Beliane, Bujumbura.

Saido aliye majeruhi hatakuwa sehemu ya mchezo wa Jumamosi hii kati ya timu yake Yanga na KMC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kadi ya mwaliko wa harusi ya Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ anatarajia kufunga ndoa Jumamosi, Machi 19 na mpenzi wake Uwera Samantha ‘Samira’.

Tayari nyota huyo yupo kwao nchini Burundi akikamilisha taratibu za ndoa hiyo na atatumia kipindi cha Ligi kusimama zikipisha ratiba za timu za taifa kama fungate kabla ta kurejea Tanzania kujiunga na Yanga.

Nyota huyo amekuwa na kiwango bora msimu huu ndani ya Yanga akihusika kwenye mabao 10 ya chama hilo kwenye Ligi kwa kufunga matano na kutoa asisti nne.

WAWA, MUGALU,MORRISON KUPIGWA PANGA SIMBA…TRY AGAIN AFICHUA MAJEMBE HAYA MAPYA… RASMI…MSUVA AFUNGUKA SAKATA LAKE NA KLABU YA MOROCCO…AGUSIA MKWANJA WA PESA..TFF YATAJWA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply